Pages

Monday, 22 June 2015

THUMUNI LETU NI KUWA KARIBU NA WAKULIMA KWA KUWAPASHA HABARI MBALI MBALI

Utaweza kujua pembejeo bora na za kisasa kwa ajili ya kuboresha kilimo chako

Utaweza fahamu jembe jeo za kisasa ili uweze kwenda na wakati


Ungana nasi ili kujua masoko ya mazao yako ili uweze kuuza aida na uweze nufaika kwa kupitia kilimo.
Pia utaweza kufahamu bei za mazao kila wakati 
kwa kujulishwa kupitia  blog hii. 

Tembelea kila wakati ili uweze kunufaika nasi kupashana habari, masoko ya mazao yaliko, bei mpya za mazao pamoja na kujua pembejeo za kisasa.


PEMBEJEO ZA KISASA HUONGEZA MAVUNO SHAMBANI




Mbegu dhaifu zinahitaji uangalizi wa hali ya juu kwa sababu mkulima asipokuwa makini, zitazaa matunda yasiyo bora.
Wakulima wengi nchini wamekuwa na mazoea ya kutayarisha mashamba yao bila kufuata msingi sahihi inayozingatia kilimo bora na kusababisha wakulima hao kupata hasara.Mara nyingi hali hiyo inatokana na wakulima kutokuzingatia ushauri wa kitaalamu, kwa mfano, kilimo bora chenye tija.
Mbali na hayo ili kujua changamoto zinazoikabili sekta ya pamba kupitia kilimo cha mkataba sambamba na umuhimu wa Mfuko wa Maendeleo ya Pamba  (CDTF), Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba nchini (TCB), Gabriel Mwallo na Meneja wa CDTF, Essau Mwalukasa, wanazungumzia mambo mbalimbali yanayohusu kilimo hicho cha mkataba. Mwalukasa anasema kazi ya mfuko huo unaojumuisha wakulima, wafanyabiashara na Serikali ni kununua pembejeo za kilimo kutoka nje kwa manufaa ya wakulima.
Akizungumzia changamoto zinazowakabili wakulima kupitia kilimo cha mkataba,  Mwallo anasema kilimo cha mkataba kinawasaidia wakulima kupata dawa za mimea na mbolea, mazao bora kutokana mbegu bora wanazopewa wakulima.Mwallo anaeleza kwamba mbegu dhaifu inahitaji uaangalizi wa hali ya juu kwani inazaa matunda yasiyo na ubora. “Gharama za utunzaji wa mbegu dhaifu ni kubwa kwa kuwa mkulima atalazimika kununua dawa nyingi ili kupata mbegu bora,” anasema.
Ameongeza kuwa iwapo mmea dhaifu utakosa dawa hizo mara kwa mara pamba itakayotoka itakuwa na weupe hafifu. Anasema kutokana na kuwapo wa dawa zenye kiwango cha chini, itamlazimu mkulima kuingia gharama zaidi kununua dawa.Kaimu Mkurugenzi huyo wa TCB, anasema ili kupata mmea bora wataalamu wanashauri mkulima kupanda kiasi cha mbegu takribani 22,200 kwa ekari moja.  “Kwa mbegu bora mkulima anaweza kurudia mara mbili kuweka dawa ya kuzuia wadudu, lakini kwa mbegu dhaifu itamlazimu mkulima kurudia mara kwa mara kwa kiwango cha  asilimia 85,” anasema.
Kuhusu changamoto ya uhaba wa mvua, Mwallo anasema: “Kilimo chetu nchini Tanzania kinategemea mvua kwa asilimia 100, lakini kwa bahati nzuri zao la pamba ni kati ya mazao yanayohimili ukame.”Mwallo anasema CDTF imelenga kusimamia maendeleo ya pamba sambamba na kuitangaza kwa ushirikiano na TCB na Kampuni ya Usambazaji wa Pembejeo nchini (MUKPAR).
Kabla ya mfuko wa CDTF, TCB ndiyo iliyokuwa na jukumu lote la kusimamia na kuendeleza sekta ya pamba katika suala zima la kulima, masoko na utangazaji. Lakini baada ya mabadiliko ya sheria,TCB ilipewa jukumu la kusimamia maendeleo ya sekta hiyo ya pamba.“Baada ya Serikali kuanzisha sera ya ubinafsishaji wadau kutoka sekta binafsi walitakiwa kushiriki katika kuendeleza sekta ya pamba nchini. Sasa kutokana na hili ikazaliwa CDTF ambayo inaundwa na wakulima wa pamba,” anasema Mwallo.
Akizungumzia dawa ya Bamesrini, Mwallo anasema dawa hiyo ililalamikiwa na kufanyiwa uchunguzi na Taasisi ya Uchunguzi wa Mbegu za Kilimo (PPRI)na kugundua kuwa haikuwa na tatizo. “Haikuwa na tatizo isipokuwa ilikuwa na ujazo wake ulikuwa ml120 badala ya ml160. Hii ilisababisha matatizo wakati mkulima akichanganya dawa hiyo na maji ambapo maji yanakuwa mengi zaidi kuliko inavyotakiwa,” anasema.
Kaimu Mkurugenzi wa TCB anaeleza changamoto nyingine wanazokumbana nazo kuwa ni baadhi ya wakulima kuchanganya pamba na mchanga ili kuongeza uzito. Akielezea namna nzuri ya kuweza kurekebisha upungufu uliyopo kwenye mfuko huo, Mwalukasa amesema mfumo mzuri unapaswa kuwapo wa kusambaza pembejeo kwa wakulima. “Ingekuwa vyema wadau wakae pamoja na kupata mfumo mzuri wa kuendesha mfumo huu. Ninaamini kwa pamoja tunaweza kupata suluhisho zuri,” anasema.

Wakulima wa tangawizi walilia pembejeo za kisasa

September 6th, 2011 | by Editha Karlo
WAKULIMA wa zao la Tangawizi katika kijiji cha Munzeze kilichopo katika Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma wameiomba serekali kuwasaidia kuwapatia pembejeo za kilimo za kisasa kwa mkopo wa bei nafuu ili kuondokana na kilimo cha jembe la mkono wacholima sasa.

Wakizungumza nami kijiji hapo baadhi ya wakulima hao wa zao hilo la Tangawizi walisema kuwa tangawizi ni zao lisilo na gharama katika kuanzia hatua ya kuandaa shamba hadi kufikia kuivuna kwa zao hilo limekuwa likistawi mahali popote penye maji ya kutosha  bila ya matatizo hata usipoweka mbolea.

Mkulima wa zao la tangawizi katika kijiji cha Lusesa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma; akiichambua tangawizi yake shambani baada ya kuivuna
Philibeth Ndayasunse ni mkulima wa zao hilo la tangawizi kijiji hapo kwa miaka miwili mpaka sasa  yeye alisema kuwa tangawizi ni zao ambalo wanalilima bila ya kutumia gharama kubwa tatizo lao ni wanalima kwa kutumia jembe la mkono hulazimika kulima eneo dogo kwa muda mrefu tofauti na kutumia trekta au power tiller ambazo zinalima eneo kubwa kwa muda mfupi.
“Najua wengi wamezowea kuona tangawizi ikilimwa Tanga, Zanzibar na maeneo mengine; hata sisi huku Kigoma tunalima zao hili tunaomba serekali yetu itukumbuke na sisi wakulima wa zao hili la tangawizi huku munzeze kwa kutupatia mikopo ya pembejeo kwa bei nafuu ili tutoke kwenye kilimo hiki cha jembe la mkono tulime kilimo cha kisasa” alisema mkulima huyo.
Ndayasunse alisema kuwa zao la tangawizi linafaida kubwa ukilima robo heka kama hazijaharibika sana unaweza kuvuna hata gunia kumi ambapo wao wanauza kwa bei ya jumla kilo moja shilingi 1000 kwa bei ya jumla na kwa bei ya rejareja kilo moja ni shilingi 2000 nasoko lao kubwa lipo kigoma mjini na mwanza.
Mkulima huyo aliiomba serekali kuwasaidia wakulima wa zao hilo kijjini hapo pembejeo za kisasa kwa mkopo nafuu kama vile trekta, powertiller kwani hicho ndo kilio chao ili waweze kulima zaidi tangawizi na pia kutoka kwenye jembe la mkono ambalo tija yake ni ndogo sana pia walihitaji zaidi wataalamu wa zao hilo ili waweze kuwapa ujuzi zaidi wa kulima zao hilo la tangawizi.
- See more at: http://www.jamiiforums.com/blog/wakulima-wa-tangawizi-huko-kigoma-walilia-pembejeo-za-kisasa/#sthash.WqGeAa7D.dpuf

"ANGALIA JINSI KILIMO CHA NYANYA KILIVYONIKOMBOA"



HIVI ndivyo anavyosema  mkulima wa nyanya kutoka katika kijiji cha Mangalali,  bwana Paschal Sichalwe  baada ya kuanza kubadili mbinu za kilimo za kizamani na kuanza kutumia mbinu za kisasa  alizozipata kupitia mafunzo yanayotolewa na mradi wa Muunganisho Ujasiriamali Vijijini (MUVI)
Mjasiriamali huyu mdogo anaelezea namna  ambavyo  mradi wa MUVI ulivyoonesha  njia ya kuelekea kwenye mafanikio kwa kutoa mafunzo ya kilimo bora, kuboresha njia za mawasiliano baina yao pia  jitihada zinazofanywa katika kuwaunganisha na  masoko mbalimbali ya ndani na nje ya nchi
Mradi wa MUVI   kwa kushirikiana na viongozi wa shirikisho la  wakulima wa nyanya wamefanya ziara za ndani na nje ya nchi katika harakati za kutafuta masoko zaidi, katika hatua za awali uongozi huo umefika nchini Kenya, Malawi na hatimaye Zambia  hii ikiwa ni kwa upande wa masoko ya nje
Masoko ya ndani, mradi wa MUVI ambao  pia umeimarisha kitengo chake cha biashara na masoko wameangalia masoko ya ndani ya nchini  na kugundua kuwa kinachosababisha nyanya kushuka bei ni kukosekana  kwa taarifa za biashara na masoko kutoka katika ngazi zote.
Katika kutatua tatizo hilo tayari mtandao wa mawasilano  kutoka  mikoa yote Tanzania zitakuwa zikipatikana ili wazalishaji wa nyanya waweze kufahamu soko liliko.  Wakulima wanapopata taarifa za biashara na masoko inakuwa rahisi kwao kufanya maamuzi ya soko. Pia matumizi ya mbao  za matangazo kwa kushirikiana na redio country fm88.5 fm na Uplands redio 89.0 fm wajasiriamali vijijini wataweza kupata taarifa za biashara na masoko.
Aidha bwana Sichalwe ambaye ameanza kuvuna  nyanya alizopanda kitaalamu akitumia mbegu bora aina ya Eden inayozalishwa na Kampuni ya Monsanto anasema kuwa ameanza kuona  faida kwani mara ya kwanza ameweza kuchuma tenga 33 ilihali msimu mzima uliopita katika shamba hilo hilo lenye ukubwa wa  nusu ekari  kwa ujumla alivuna kiasi cha tenga 56 tu.
“Msimu uliopita nilitumia mbegu  aina ya  ONXL katika shamba la nusu ekari  michumo yote nilipata  tenga  56 tu lakini sasa mchumo mmoja nimewezakuchuma  tenga 33 na nategemea kuchuma kiasi cha tenga   26 katika mchumo  wa pili.” anasisistiza Sichalwe.
Msimu uliopita nilitumia kiasi cha shilingi 532,800 ikiwa ni gharama nzima ya uzalishaji  kwa upande wa pembejeo pamoja na nguvukazi,mapato ilikuwa 606000, msimu huu nimetumia kiasi cha shilingi 570,900 kwa ajili ya pembejeo na nguvu kazi nategemea kupata kiasi cha shilingi 1,045,000 Kwa mtizamo wa haraka haraka,  bwana Sichalwe ameanza kuona faida katika kilimo cha nyanya kufuatia mchanganuo huo alioufanya.
Sichalwe ambaye pia pamoja na zao la nyanya hujishughulisha na kilimo cha alizeti na mahindi, katika hatua nyingine amewezakuimarisha biashara ya kuuza bidhaa ndogondogo kwenye  kibanda chake ambapo pia anaamini kuwa kuna siku atakuwa mjasiriamali mkubwa.
Awali Sichalwe alikuwa akilima kwa mazoea bila kutunza kumbukumbu  kuanzia uzalishaji hadi sokoni lakini baada ya mradi wa MUVI kupisha hodi kijijini kwake na kufundishwa kilimo cha kibiashara na njia rahisi ya kuandaa mpango biashara sasa ameweza kutunza taarifa zake za kilimo tangu hatua ya mwanzo hadi mwisho, hapo ndipo anapoweza kubaini mapato na matumizi katika shughuli  nzima.
“Wajasiriamali wengi wanasahau kuweka kumbukumbu  za uzalisha katika  shuguli zao wanazofanya kila siku, mali bila daftari hupotea bila kujua,kila unachofanya inakupasa uandike, kuna wengine pia hujisahau wao wenyewe, mfano akipalilia nyanya mwenyewe au akipanda hujisahau katika kipengele cha malipo ile ni nguvu kazi inapaswa kulipwa na hili linawezekana kama utakuwa umeandika”anasema.
Katika hatua nyingine Sichalwe anaamini kuwa baada ya kupata mavuno mengi na yakutosha msimu huu anatarajia kuanza kilimo cha umwagiliaji  ambacho anaamini kuwa kitamkomboa zaidi.
Pamoja na mambo mengine Sichalwe  anampango  wa kuimarisha kilimo cha ufugaji kwani tayari amenunua mbuzi  5 mara baada ya kuuza nyanya.  Idadi hiyo anaona kuwa haitoshi hivyo  anategemea kuongeza kiasi hicho  hadi kufikia mbuzi 20.
Si hapo tu Sichalwe anaamini pia kwa kuzingatia mbinu za kisasa alizozipata kupitia mradi wa MUVI kufikia mwishoni mwa mwaka  atakuwa amenza ujenzi wa nyumba ya kisasa ya kuishi.
Katika kuhakikisha kuwa Sichalwe na wajasiriamali wengine wanaozalisha  nyanya kijijini hapo wanapata mafanikio,  mradi wa MUVI umemtuma ofisa masoko  wa mradi huo kuzungumza na  na wakulima wa nyanya  katika hali ya kuwaondoa hofu hususani kwenye kipengele cha masoko.
Akizungumza na wajasiriamali wa Mangalali hivi karibuni muda mfupi mara baada ya kuunda kamati ya biashara na masoko, Ofisa masoko wa mradi, bwana Fredy Mumbuli amesema, wakulima wanategemea zaidi soko la Kariakoo na Ilala.Wafanyabiashara hawa huwa wanakimbilia katika masoko haya kwa kukosa taarifa nzuri za masoko.
“wajasiriamali hupeleka nyanya kwa wingi katika masoko hayo kwa kukosa taarifa  sahihi za masoko hali inayoplekea kushuka kwa bei ya bidhaa husika,wakulima wote nchini wakishavuna hufikiria kuuza bidhaa zao Dar es salaam  jambo ambalo si sahihi hata kidogo.”alisema Mumbuli. na kuzidi kubainisha kwamba kuwa kuna wakati  kunakuwepo na uhitaji mkubwa wa nyanya Morogogo, Arusha au Dodoma  na hata wakati mwingine Iringa
Mkulima anayezalisha nyanya Morogoro akipata taarifa za soko zuri la nyanya  Iringa anaruhusiwa kufanya  biashara  vivyo hivyo na kwa upande wa mkulima wa Arusha, Kilimanjaro na mikoa mingine inayolima zao hilo.
Hili litawezekana mara baada ya kuimarisha njia za upashanaji habari kupitia  vyombo vya habari na mbao za matangazo ambazo tayari mradi wa MUVI umejenga katika kata  16 mkoani Iringa na Njombe.
Kitengo cha habari  na mawasiliano kitakuwa kikifanya kazi  kwa ushirikiano mzuri na kitengo cha biashara na masoko katika kuwapatia wakulima taarifa za biashara na masoko.

MAFUNZO YA MSINGI YA KILIMO BORA CHA UFUTA - AMSHA



Taasisi ya Amsha – www.amsha.org, wameandaa mafunzo ya msingi ya kilimo bora cha ufuta, terehe 14/03/2015.
 
LENGO
Kuwapatia wakulima kanuni na taratibu za msingi juu ya kilimo cha ufuta katika Nyanja zifuatazo;

• Jinsi ya kuandaa shamba kitaalamu kwa ajili ya kilimo cha ufuta (kulima,uchaguzi mbegu na kupanda).

  • • Jinsi ya kulisimamia shamba husika/ Usimamizi wa shamba kabla ya mavuno
  • Matumizi ya mbolea
  • Jinsi ya kufanya palizi
  • Kutibu na kudhibiti magonjwa
  • Usimamizi wa shamba baada ya mavuno
  • Njia bora za kuvuna na nyezo
  • • Huifadhi wa zao la ufuta baada ya mavuno kwaajili ya soko husika.

MAHALI
Ubungo plaza (Dar-es-salaam)
Gharama ya mafunzo ni shilling 30,000/= ( ilipwe kabla ya terehe 04/03/2015). Malipo yafanyike kwa Mpesa kupitia namba 0755 – 428353 (namba hii maalumu kwa malipo tu).
 
MAWASILIANO
0717-806888 / 0659-339905/ 0716-966447, barua pepe: pr@amsha.org cc: info@amsha.org
- See more at: http://agriprofocus.com/post/54ddbca8d58d834f0943055d#sthash.Q9o5wHSg.dpuf - See more at: http://agriprofocus.com/post/54de1959d58d834f09430566#sthash.DH7rpX4H.dpuf
 
SOURCE; www.amsha.org

Wakulima wa Pareto Mbeya walipwa Pesa zao



Kampuni ya Pareto Tanzania (PCT), imewalipa zaidi ya Sh4.4 bilioni  wakulima wa pareto katika mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na Arusha kuanzia Agosti mwaka jana hadi Machi mwaka huu baada ya kununua tani 2,300 za zao hilo, imeelezwa.
Meneja wa PCT, Martin Oweka alisema hayo alipoulizwa hatua za kampuni yake kuondoa kero ya wakulima wa zao hilo waliokuwa wakilalamikia msimu uliopita kutokana na baadhi ya kampuni kuchukua mazao yao na kuingia mitini.
“PCT Iliwalipa fedha zote baada ya kupima sumu ya pareto ambayo mwaka huu imeongezeka ubora wake na kusababisha wakulima wapate fedha nyingi ikilinganishwa na msimu uliopita,” alisema Oweka.
Mkulima wa zao hilo katika Kijiji cha Igale, Mbeya Vijijini, Admina Mlonzi alisema wakulima waliochuma maua yaliyochanua na kuyakausha vizuri waliyauza kwa Sh2,400 kwa kilo moja jambo ambalo linaongeza kasi ya kuboresha uvunaji, ukaushaji na uuzaji ndani ya muda unaopangwa.
Vijiji vyenye wakulima waliopata fedha nyingi baada ya kuuza pareto bora ni pamoja na Itale, Igale, Nzoho na Isongole mkoani Mbeya, wakati upande wa Njombe ni Kitope, Mulondwe na vingine vipo mikoa ya Manyara na Iringa.
Mkulima Laurent Shila wa Kijiji cha Itale Mbeya Vijijini, alisema wakulima wa pareto waliofuata maelekezo ya wataalamu katika uchumaji wa maua, wamepata fedha nyingi na kuna uwezekano wa miaka ijayo wakulima wengi wakalipenda zao hilo.
Kiwanda cha pareto kilichopo Mufindi, kina uwezo wa kusindika tani 6,000 kwa mwaka, lakini mwaka huu kimepokea tani 2,300  zilizolimwa na wakulima 25,000 hivyo uongozi wa kiwanda hicho kudhamiria kuwahamasisha wakulima kulima zao hilo kwa kufuata kanuni bora ili wanufaike.

BEI ZA MAZAO

Kutokana na tafiti mbalimbali ziliofanywa imegundulika kuwa wakulima wengi wanauza mazao yao kwa bei ya chini hasahasa katika msimu wa mavuno kutokana na kutokuwa na taarifa sahihi za masoko ya bidhaa zao
Shamban solutions kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo tutakuwa tunakuletea bei za mazao kutoka katika mikoa mbalimbali ya tanzania na afrika mashariki kwa ujumla 
                        - Bei muafaka kwa Wakati muafaka -

BEI MPYA ZA MAZAO KUTOKA KATIKA MIKOA MBALIMBALI YA TANZANIA(Tshs/kg))
TAREHE 26/12/2013 

Mkoa
Maharage     
Mahindi     
Mchele     
Mtama   
 Ngano              
Ulezi              
Viazi Mviringo 
Arusha
1100 -1450
500 - 520
1100-1500
550 - 600
700 - 850
980 - 1000
700 - 750

Babati
1400 - 1450
450
1300-1500
350 - 420
750 - 800
900 - 950
650 - 1000

Bukoba
1300 - 1600
680 - 700
1000-1100
450 - 500
900 - 1200
1100 -1200
560 - 600

Dsm
1300 - 1800
480 - 520
800 - 1300
600 - 700
1000 -1200
1200 -1500
500 - 650

Dodoma
1300 - 1500
540
1300-1500
540

1000 -1500
400 - 600

Geita
1400
720
1000
650

1400
600

Iringa
1000 - 1400
360 - 370
1200-1500
800
700 - 1000
1000 -1200
500

Kigoma
1500
670
1000-1200
1500

1500
800 - 1000

Lindi
1400 - 1700
550 - 600
1100-1400
500

1200 -1700
620

Mbeya
950 - 1300
480 - 500
900 - 1300

800 - 1000
750 - 900
250 - 260

Morogoro
1400 - 1500
480 - 560
1000-1300
1200
1300
1500
360 - 410

Moshi
1400
510
1300

1200
1700
1000

Mpanda
1000 - 1700
500
800


800
1500

Mtwara
1200 - 1600
550 - 570
1100-1200
1200
1200 - 1500

800

Musoma
1300
760
1280
680

1350
1250

Mwanza
1400 - 1500
650 - 700
950- 1000
1200 - 1500
700
1400
550

Njombe
1200
550
1800

700 - 750
1200
350

Shinyanga
1400 - 1500
500
1000-1200
350 - 375
1000 -1200
1300
530 - 590

Singida
1300 - 1600
480 - 500
1000-1200
500 - 540

900 - 950
800 - 850

Songea
900 - 1000
320
1000-1800


1000
600

Sumbawanga
900 - 1800
390 - 420
1000-1200

720 - 750
900 - 1050
650 - 750

Tabora
1500 - 1700
540 - 550
850 - 1000
1000
1200
1000
700

Tanga
1200 - 1300
490 - 500
1200-1250
550 - 600
900 - 950
1300
500 - 560




























Published by Shambani Solutions Tanzania

MKULIMA FUNGUKA KWA KUFAHAMU JINZI YA KUBORESHA KILIMO CHAKO

MKULIMA FUNGUKA KWA KUFAHAMU JINZI YA KUBORESHA KILIMO CHAKO